Pages

Saturday 3 May 2014

JE KADINALI NI KIONGOZI MKUU WA KANISA KATOLIKI NCHINI

HIVI karibuni, gazeti la Daily News (ISSN 0856-3812, No. 11,152) katika ukurasa
wake wa
 mbele liliandika hivi, (..“in D’Salaam, the Head of Roman Catholic Church in 
Tanzania,
 Polycarp Cardinal Pengo, trumped wisdom for personal gratification and 
welfare of the
 nation at large”..).
Jioni Machi 14, 2014, nilimsikiliza Januari Makamba akitoa mchango wake wa
maoni kwenye
Bunge la Katiba. Wakati anahitimisha, alituasa tuheshimu maoni ya viongozi
wa dini
waliopendekeza Serikali mbili, akiwemo Polycarp Kardinali Pengo.
Hii ilikuwa wiki moja baada Samuel Sitta kuwatembelea Polycarp Kardinali Pengo
 pamoja na
 Mufti wa Tanzania, Issa Shaaban Simba.
Kwa asiyeujua muundo wa Kanisa Katoliki, ikitangazwa kwamba Samuel Sitta
katoka kwa
Mufti kisha amekwenda kwa Polycarp Kardinali Pengo, ni rahisi kudhani ilikuwa
ni ziara ya
 kuwatembelea viongozi wa dini wa ngazi ya kitaifa.
Hata mimi utotoni nilikumbatia dhana kwamba, Laurean Kardinali Rugambwa
ndiye aliyekuwa
 Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini, kwani aliwapa daraja maaskofu 26, wakati
Polycarp Kardinali
Pengo amekwishawapa maaskofu 24.
Nilipokumbatia dhana ya pili kwamba Mkuu Kanisa nchini ni Rais wa Baraza la
 Maaskofu,
nikajiona nimetumia hoja ya kisomi zaidi!
Nilipoanza kusoma nyaraka rasmi za kanisa, hasa Sheria za Kanisa ziitwazo
Code of Canon 
Laws”, ndipo nikagundua sikuwa na ukweli wowote katika zile dhana mbili.
Hizi “Canon Laws” ibara zake hutajwa hivi, Can. 381, zinatosha kumwelewesha
 yeyote
muundo wa Kanisa Katoliki. Zinataja mamlaka ya askofu, askofu-mkuu,
kardinali,
 rais wa
baraza la maaskofu na zaidi.
Hakuna ibara inayoonyesha kwamba kuna “mkuu wa kanisa”, au “msemaji
wa kanisa” katika
nchi yoyote.
Kinyume chake, sheria ya kanisa, Can. 381(1) na Can. 391(1), zinasema
kwamba askofu
 jimboni, ndiye mkuu na mwenye madaraka jimboni.
Ibara hii inatokana agizo la mkutano wa maaskofu uitwao Vatican II,
uliotoa hati iitwayo
Lumen Gentium” ibara ya 27, isemayo kwamba, askofu jimboni ni
mwakilishi wa Yesu na
 si mwakilishi wa Papa au chombo chochote.
Vilevile, hakuna andiko la kanisa linalotaja maneno “makao makuu”.
Badala yake jengo la
 kanisa liitwalo “Cathedral” ndilo lenye mamlaka ya uaskofu.
Kwa wale wanaopenda neno “makao makuu”, basi afadhali waseme

Cathedral” ndiyo “makao
 makuu” ya kanisa jimboni.
Pale Roma, “Cathedral” ni kanisa liitwalo “St. Lateran’s archbasilica”.
Kumbe, makao “makuu
ya Kanisa Katoliki duniani”, siyo anakoishi Papa yaani kule Castle
Gandolfo au pale Vatican,
 bali ni hapo “St. Lateran archbasilica”.
Hata kanisa maarufu lililopo Vatican, yaani “St. Peter’s basilica”,
lina hadhi ndogo iitwayo
“basilica”, wakati hili la “makao makuu” linaitwa “arch-basilica”,
 hadhi kubwa kuliko makanisa
yote Katoliki duniani.
Ibara ya 390 na 436(3) ya sheria za kanisa, zinamkataza askofu (bishop)
 pamoja na
askofu-mkuu (arch-bishop) wasiendeshe misa kwenye “Cathedral
bila ruhusa ya askofu
mwenye jimbo.
Hivyo, Polycarp Kardinali Pengo au askofu Tarcicius Ngalalekumtwa,
hawawezi kuendesha
misa kwenye “Cathedral” ya Ifakara, bila kwanza kuruhusiwa na askofu
 Salutaris Libena.
Pia, kwa kutumia sheria, Can. 763, askofu wa jimbo, mfano pale Ifakara,
amepewa mamlaka
na Papa kumpiga marufuku askofu yeyote duniani asihutubie lolote jimboni
Ifakara ikihitajika
 kufanya hivyo.
Mwaka 2004, Joachim Kardinali Meisner, alitumia ibara hii kumkataza askofu
Jacques Gaillot
asiingie jimboni Cologne, kwani alikwishachokwa kuigawa nchi kwa kauli zake
 alizoziita “ni
maoni yake binafsi”.
Nimechagua ibara hizi chache kuonyesha mamlaka ya askofu, uone kwamba,
hakuna askofu
 hata mmoja nchini aliye juu ya mwingine.
Sasa tuone ukardinali ni nini?
Mkatoliki akitaka utumishi wake utambulike rasmi kikanisa, lazima atasajiliwa
au kusimikwa
 kwenye kundi linalotambulika. Mara nyingi huwa ni jimboni au kwenye jumuiya
ziitwazo
 “religious”.
Zamani kila aliyesimikwa hivyo aliitwa “kardinali”. Lakini kuanzia karne ya tisa,
 neno
“kardinali” lilibaki kutumika tu kwa walioitwa na Papa wakahamia na kusimikwa

 upya Roma.
Padri aliyehamishiwa Roma, huko alisimikwa kwenye kanisa lililoitwa titular church”.
Hiyo ikawa aina ya kwanza ya makardinali, wakijulikana kama “cardinal-Priest”.
Baadaye mashemasi nao wakawa wanahamishiwa Roma, huko wakapewa vituo
 vilivyoitwa
deaconia”.  Ikawa aina ya pili ya makardinali waitwao “Cardinal-Deacon”.
Kazi za Papa zilipoongezeka, akahitaji msaada wa maaskofu kutoka majimbo
 jirani yaliyoitwa
 “Suburbicarian Diocese”. Hali ya maaskofu hawa kuwa karibu na kuhitajiwa
Roma,
kukawafanya waitwe “Cardinal-Bishop”.
Hizi ndizo aina tatu za makardinali. Zipo hadi leo, yaani “Cardinal-Deacon”,
 “Cardinal-Priest” na “Cardinal-Bishop”.
Kuanzia mwaka 1150, Papa alianza kuwaita makardinali kwenye vikao vya
kumshauri,
ambavyo hadi leo vinaitwa “Consistory”.
Mwaka 1179, haki ya kumchagua Papa mpya, ikaacha kuwa ya wanajimbo
 wengine wa
Roma, bali ikabaki kwa “makardinali” tu kwenye mkutano unaoitwa “Conclave”.
 Mwaka 1975,
 Papa Paul VI alifupisha umri wa kardinali kuhudhuria “Conclave”, yaani chini ya
 miaka 80.
Tumeona kwamba, kitendo cha kupewa ukardinali na Papa, ni uhamisho wa
 kwenda Roma.
Uhamisho huo unamfanya awe mwanajimbo wa Roma, ambaye kama haishi
Roma, basi
 kokote aliko duniani anafanya umisionari.
Ile aina ya “Cardinal-Bishops” bado hupewa lile kanisa liitwalo “Suburbicarian
 Diocese”.
Siku hizi “Cardinal-Deacons” hupewa hata yale makanisa, “titular church”.
Ile aina ya “Cardinal-Priest”, wengi hawaishi Roma kwa sababu ya umisionari
wao mbali na
Roma. Mmojawapo ni Polycarp Kardinali Pengo, anayeongoza Jimbo la
Dar es Salaam,
 lililo kilomita 6043 kutoka Roma.
Je, mtu anapewa ukardinali baada ya kufikia ngazi ipi ya utumishi? Teodolfo
Kardinali
Mertel, alipewa ukardinali Machi 15, 1858 akiwa hajapata hata ushemasi.
 Machi 20, 1556
Reginald Kardinali Pole alikuwa ameshakuwa kardinali kwa miaka 20 na
ameshashiriki
Conclave” tatu akiwa hajawa padri.
Kuanzia Februari 2, mwaka 1983, Papa John Paul II aliwapa ukardinali
mapadri saba,
waliobaki na upadri wao bila kuwa maaskofu.
Watano kati yao wameshafariki ambao ni  Henri Kardinali de Lubac,
Avery Kardinali Dulles,
 Aloys Kardinali Grillmeier, Joseph Kardinali Congar, Leo Kardinali Scheffczyk.
 Wawili kati yao
 wako hai, yaani Roberto Kardinali Tucci na Albert Kardinali Vanhoye.
Papa Benedict XVI, naye ana mapadri wanne aliowapa ukardinali bila kuwa
maaskofu. Watatu
wamekwishafariki, ambao ni Domenico Kardinali Bartolucci, Urbano
Kardinali Navarrete,
 Umberto Kardinali Bett. Aliye hai ni Josef Kardinali Becker.
Roman Curia” ni jopo linalomsaidia Papa kuendesha kanisa lote duniani.
Karibu timu
yote “Roman Curia” huripoti shughuli zake kwa “Secretariet of State”.
Hivyo, “Secretariet of State” ana majukumu mazito ndani na nje ya Kanisa,
 kwani Papa
 anaweza kusifiwa au kulaumiwa ndani na nje ya kanisa kwa sababu tu ya
utendaji wa huyu
 “Secretariet of State”.
Nafasi hii ya “Secretariet of State” sasa inashikwa na Pietro Kardinali Parolin,
aliyeachiwa na
Tarcisio Kardinali Bertone.
Wote Kardinali Bertone na huyu Parolin ni maaskofu. Lakini mwaka 1848,
 nafasi
hii ilisimamiwa vizuri na Giacomo Kardinali Antonelli, ambaye alikuwa shemasi
 tu hadi kifo
chake Novemba 06, 1876.
Papa anaweza kumpa mtu ukardinali kwa siri, yaani “Cardinal in pectore”.
Serikali ya China
 ilipomfunga askofu Ignatius Kung Pin-mei wa Shanghai, haigundua
kwamba akiwa humo
 gerezani alipewa ukardinali kwa siri mnamo Juni 30, 1979.
Kardinali yeyote, kama alivyo Polycarp Pengo, siyo mwakilishi wa nchi
 kama Tanzania,
kwani, hakuna jimbo wala parokia inayoitwa Tanzania.
Tumeona kwamba ukardinali ni kuwa mwanajimbo wa Roma au jirani na Roma
 (suburbcarian). Hivyo, hata inavyoelekeza sheria ya kanisa, Can. 357(1),
 kardinali
ni mwakilishi wa parokia yake pale Roma yaani “titular chuch”, ambayo ya
Polycarp Pengo
 pale inaitwa Nostra Signora de La Salette.
Lakini ibara hiyo 357(1), bado inamdhibiti kardinali kwamba, hata hiyo parokia yake
pale Roma, haruhusiwi kuiingilia kiutawala, kiuendeshaji au kinidhamu.
Hivyo, eneo pekee duniani ambako Polycarp Pengo ana mamlaka ya uchungaji,
utawala, uendeshaji au nidhamu, ni ndani ya mipaka ya Dar es Salaam tu
 (rejea, Can. 381(1).
Wakati mabaraza ya maaskofu yanashamiri duniani, baadhi ya maaskofu
waliitaadharisha Vatican kwamba, ama baraza zima au rais wa baraza hilo,
ataweza kujikuta anaingilia ukuu wao jimboni na kugeuka kuwa mkuu nchini.
Hivyo, Papa aliiweka ibara ya  455(4) makusudi kulinda huo ukuu wa askofu
wa jimboni, ili asiingiliwe kwa namna yoyote na baraza zima au rais wa baraza
 la maaskofu.
Hivyo, ibara hii inatosha kukuthibitishia kwamba, rais wa baraza la maaskofu,
si kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini, wala si mkuu wa maaskofu nchini.
Hivyo, Rais wa TEC, Askofu Tarcicius Ngalalekumtwa, naye eneo pekee la ukuu
wake, ni mipaka ya Jimbo la Iringa tu.
Mkutano wa makardinali wote duniani na Papa yaani “consistory”, hauna mamlaka
ya kutoa tamko kisha liitwe kuwa ni la Kanisa Katoliki duniani. Huo ni mkutano
 wa
askofu wa Roma na wanajimbo wake.
Wakati mkutano wa maaskofu wote duniani na Papa, ndicho chombo kikuu kupita
 vyote kiitwacho “magisterium”, chenye mamlaka ya kuamua lolote ndani ya
 Kanisa Katoliki.
Ibara ya 1121 ya Katekism ya Kanisa Katoliki inasema, askofu haachi
kuwa askofu
 hadi kifo chake, hata akijiuzulu madaraka.
Lakini ukardinali ni tofauti. Padri Louis Billot alikuwa kardinali kwa miaka 16
,alipojiuzulu
 ukardinali Septemba 21, 1927, akaacha kuwa kardinali.
Hivyo, uaskofu ni nafasi ya juu zaidi na nyeti zaidi ndani ya Kanisa Katoliki,
kuuzidi ukardinali.
Lakini, siku hizi, msemaji akishamtambulisha kardinali, anafuata askofu-mkuu,

kisha askofu, baadaye mapadri na kuendelea, halafu mwishoni anasema
itifaki imezingatiwa”!
Tumeona kwamba “Secretariet of State” wa “Roman Curia”, yaani Kardinali
Antonelli, hata upadri hakuufikia. Tumeona, kwamba hata leo, wapo hai na
wametajwa humu makardinali watatu ambao hata uaskofu hawajaufikia.
Pia, mifano mitatu ifuatayo nchini Albania, Switzerland na Italy, inakufahamisha
kwamba Papa John Paul II, amewahi kufanya jimbo liwe na padri ambaye
ni kardinali,
wakati askofu wa jimbo hilo si kardinali.
Jimbo la Chur (Switzerland), halijawahi kuongozwa na askofu ambaye ni
kardinali.
 Lakini padri Hans Urs von Balthasar wa humo, alitangazwa kwenye orodha ya
 makardinali Juni 28, 1988.
Mei 25, 1985, hayati askofu Antonio Mistrorigo wa Treviso (Italy), alishuhudia
padri wake Pietro Pavan akipewa ukardinali wakati mwenyewe hakuwahi kuwa
kardinali.
Novemba 26, 1994, hayati askofu Franco Illia wa Shkodre (Albania), alishuhudia
padri wa jimbo lake yaani Mikel Koliqi akipewa ukardinali wakati yeye mwenyewe
 hakuwahi kuwa kardinali.
Kumbe, yaliyotokea Albania kwa Kardinali Koliqi, yanaweza kabisa kujirudia
Tanzania, yaani padri wa jimbo moja tu nchini anakuwa kardinali, wakati hakuna
askofu hata mmoja nchini aliye kardinali.
Hivi, ikitokea hivi, halafu huyo padri ambaye ni kardinali, akusanyike na maaskofu
wote nchini ambao si makardinali, je, wapenzi wa ile “itifaki”, wataizingatia vipi ile itifaki
yao?
Ukitaka kuvijua “vyeo” ndani ya Kanisa Katoliki, sharti utulie na kuvisoma.
Vinginevyo,
 unaweza kuhutubia tuheshimu mawazo ya mwenye “cheo” fulani, ukidhani
ndiye mkuu
 hapa nchini, kumbe sivyo.

1 comment: