Pages

Saturday 31 January 2015

Padri Wootherspon: Kukutana na Dr. Slaa ni sawa nakukutana Mandela au Nyerere

Padri kutoka Hong kong aliyekuja Nchini kuhimiza kampeni ya kuwazuia Vijana kuacha kusafirisha dawa za kulevya katika Majimbo ya China ya Guangzhou, Macau na Hong kong, Amesema kukutana kwake na Dr.Slaa ni sawa nakukutana na kiongozi kama Mandela au Nyerere.

Alisema hayo alivyokaribishwa Nyumbani kwa Dr.Slaa nakufanya nae Mazungumzo yaliyochukua Dk.90.

Chanzo: Mwananchi

======
Kauli ya Dr. Slaa mwenyewe:
Quote By Dr.W.Slaa View Post
WanaJF,

Awali ya yote Napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru sana Father Wootherspon, kwa kutengeneza nchi yetu, nasa kutembelea baadhi ya Familia za Vijana wetu waliofungwa kwenye magereza mbalimbali za HongKong na China. Mwenyezi Mungu amrudishie Maradufu kwa Upendo, huruma na ukarimu wake. Fr. Wootherspon ni Mu Australia anayefanya Kazi za ki missionari HongKong. Kwa muda mrefu amekuwa Alifanya huduma zake kwenye magereza ( kama wanavyofanya viongozi mbalimbali wa Madhehebu ya Dini hata huku kwetu). Ni katika utekelezaji wa Majukumu yake ndiyo Fr. Wootherspon alipo kutana na Vijana wengi wa kitanzania, wakihangaika, na kufadhaika kwa ku kosa ndugu japo wa kuwafariji.

Ndipo Fr. Wootherspon alipoanza kujenga kwanza unafiki nao na hatimaye wakajenga Imani na aka was Kifungu ki kubwa kati ya viongozi wa Magereza na Vijana, na pia Vijana na familia zao. Amekuwa pia akiwasiliana na viongozi wa Serikali yetu katika jitihada a) kutafuta njia ya kuthibiti Vijana wengi kutoingia kwenye bias hata ya madatta ya kulevya, hasa ikizingatiwa kuwa kuna Wakati walikuwa wanakamatwa Vijana watatu/ wanne kwa wiki, b) kutafuta Mbinu za kutoa elimu kwa Vijana wanaojihuisha na bias hard ya madawa ya kulevya kwa sababu mbalimbali bila kujua yanayowasubiri mbele ya safari. Ndio maana Mara kwa mara amekuwa akituma nyaraka na hasa barua mbalimbali zilizoandikwa kwa mikononi yao wenyewe ili Vijana wenzao Waajue hali ilivyo ngumu. Fr. Amekuwa mwanachama mzuri wa JF kutoa elimu kwa Vijana wetu kama njia ya kuwaelimisha wajue pushy na Madawa ya Kulevya.

Watanzania wenzangu. Mimi nimekutana and Fr. Wootherspon. Namshukuru sana kukutana na Mtumishi wa Mungu, aliyezoea Maisha yake kuwahudumia Vijana wetu wa Makabila mbalimbali, jinsia mbalimbali , Madhehebu mbalimbali ya Dini. Kwake Yeye wote ni Watanzania, wako ugenini na wanaohitaji faraja, Upendo, huduma ndogo ndogo wanaohitaji wafungue. Wako walioko rumande, wako waliokwisha huku iwe Kifungo, kati ya miaka 3 hadi 7. Wako waliohukumiwa kifo. Wote anawahudumia, ikiwa ni pamoja na kutafuta namna ya kufikisha ujumbe kwa ndugu na familia zao huku nyumbani. Huyu ni Mu Australia asiyejua hata neno la Kiswahili, wala chembe ya Utamaduni wa Mtanzania. Anafanya kwa kusukuma na Upendo, utu na Ubinadamu. Tunaweza kutofautiana kwa Rangi, Dini au Kabila lakini hatimaye wote ni viumbe vya Mungu.

Watanzania Wenzangu, nimeandika kwa kirefu kwa kuwa ni vema tukijua wanaoangamia na Madawa ya kulevya ni Watanzania Wenzetu. Wanakamatwa na au kufungiwa au kunyongwa ni Watanzania wenzetu. Wengi wao ni Vijana wa kiume na magi tu wadogo sana, kaka zetu, dada zetu watoto wa wajumbe, wapwa, marafiki zetu tuliosoma nao, tunaotoka nao kijiji Kimoja. Ni Aibu Mu Australia anawagawa huruma, anawahudumia kwa Upendo mkubwa sisi tunapoteza muda mbele ya computer ku chat na kujadili Hoja zisizo na miguu wala mikono! Tunajiaibisha watanzania! Tusifikiri Duniani kuna siri tena, tunafanya kila kitu kizembezembe au kwa Utani.mzee wa Watu amekwenda Mpaka vijijini kufanikisha familia za Watanzania, sisi tunaifanyia Utani.

niwaombe Watanzania wenzangu, niombe tu tusipoteze muda kujadiliana na hao wanaofanyabutani na maisha ya binadamu wenzao. Mwl. Nyerere aliwahi kusema, afadhali "Mjinga" kwa kuwa anaweza kupewa elimu akaelimika. Huwezi kumwelimisha " Mpumbavu". Teachable na kujibiza na hao. Tukijibizana nao dunia inaweza isitambue kati yetu na wao " wapumbavu" ni nani.

Watanzania Wenzangu, Fr. Ameridi HongKong. Ili tu muenzi, nashauri kila mmoja wetu nafasi yeyote unayopata iwe kwenye mitandao, magazeti, kwenye vijiwe, au popote pale tutumie nafasi kuwaelimisha Vijana wetu waachane kujibu sashay na Madawa ya kulevya.

Tuwaelemishe Vijana wetu waikatae kutumika kama Punda kubebeshwa Madawa na Watu wachache ambao dhamira zao zimekufa siku nyingi. Tuwaelemishe Vijana kuwa Wenzetu hasa China, HongKong, Singapore na Indonesia hawana huruma na mtu anayebeba, mahali pengine kifungo cha chini ni miaka Saba, na jukumu ya kifo ni Jambo la kawaida.

Ndugu zangu kama ubeba kente kwenye mawili wako kwa Masai hajui itawasilisha saa ngapi, hujui utakamatwa saa ngapi. Wakati wewe unateseka mwenzako anatesa. Mitaani na magari ya Fahari. Akiishapata utajiri wake kwa njia yako wewe huna thamini tena, na ukiacha kamatwa ndio kwanza ha kujui. Achaneni na hao wanaotukana badala ya kujadili Hoja. Inawezekana " wamehamia" kwa kuwa ndio wahusika Wakuu. Sisi tuhangaikie Vijana wetu, Nguvu Kazi ya Taifa letu, ndugu na marafiki zetu.

Jukwaa letu liwe chimbuko la kuelimisha umma athari za Madawa ya kulevya na hatari ya kujiingiza kwenye biashara hii, kwa sababu yoyote ile.

Nawashukuru sana.

Dr. Slaa

No comments:

Post a Comment